1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampala. Maandamano yageuka kuwa ghasia.

13 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAO

Kiasi watu watatu wameuwawa na wengine kadha wamejeruhiwa baada ya waandamanaji katika mji mkuu wa Uganda Kampala , kufanya ghasia. Maandamano hayo yaliitishwa ili kupinga kuuzwa kwa sehemu ya msitu wa hifadhi kwa mmiliki wa kampuni mwenye asili ya Kihindi ambaye alikuwa na mpango wa kutumia sehemu ya msitu huo kwa kilimo cha miwa kwa ajili ya kutengeneza sukari.

Watu walioshuhudia wamesema kuwa hali ilianza kwa utulivu na ghafla ghasia zilizuka.

Miongoni mwa wale waliouwawa ni pamoja na mtu mmoja mwenye asili ya Kihindi ambaye alipigwa mawe hadi kufa.

Haijafahamika iwapo alikuwa anahusika na kampuni hiyo inayopingwa.