1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Waasi waomba msamaha kuhusu ukatili uliotendwa

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79U

Baada ya mapigano ya miaka 20,waasi wa Uganda katika hatua ya upatanisho,wameomba msamaha kwa ukatili waliotenda.Wajumbe wa LRA walipotembelea eneo la kaskazini,walikiri kuwa walifanya makosa na wameomba kusamehewa na wale walioathirika. Kiongozi wa LRA Joseph Kony hakuwepo katika ujumbe huo.Kony na manaibu watatu wa ngazi za juu wanasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini The Hague kwa uhalifu wa kivita.Maelfu ya watu wameuawa wakati wa vita hivyo na takriban wengine milioni mbili wamelazimika kuondoka makwao.