1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni za Uchaguzi zapambana moto Ujerumani

19 Septemba 2013

Wahariri katika magazeti ya leo(19.09.2013)wamejishughulisha zaidi na kampeni za uchaguzi hapa Ujerumani, mzozo wa silaha za sumu nchini Syria, pamoja na Ujerumani kutimiza miaka 40 katika Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/19kXy
Ein Mann geht am 30.08.2013 in Oberursel (Hessen) an einer Plakatwand mit den Wahlplakaten der verschiedenen Parteien vorbei. Am 22. September findet neben der Bundestagswahl auch die Landtagswahl in Hessen statt. Foto: Arne Dedert/dpa
Mabango ya uchaguzi UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa

Mhariri wa gazeti la Volksstimme la mjini Mag-denbug anazungumzia kuwa kwa muda mrefu kampeni za uchaguzi nchini Ujerumani zimekuwa hazina msisimko. Mhariri anaeleza .

Sasa kampeni hizo ziko katika hali ya kusinzia. Maoni ya wapiga kura ya hivi karibuni yanatoa mtazamo wa mkwamo kati ya serikali na upinzani. Hatua za mwisho zinaonesha hali ya kutoeleweka.

Supporters of German Chancellor Angela Merkel and head of German Christian Democratic Union CDU hold electoral placards reading 'Angie' during her visit ahead of the upcoming September 22 legislative elections, on September 7, 2013 in Oranienburg. AFP PHOTO / JOHANNES EISELE (Photo credit should read JOHANNES EISELE/AFP/Getty Images)
Katika mkutano wa kampeni wa CDUPicha: JOHANNES EISELE/AFP/Getty Images

Chama cha FDP kinapambana kuwania kujioko kisiasa na kinaomba kura kutoka kwa wale ambao hawajaamua wapige kura zao wapi na pia kwa wapigaji kura ambao watapigia kura muungano wa vyama vinavyotawala. Chama cha kijani kinajaribu kujitoa kutoka katika mambo yaliyotokea hapo zamani. Mjadala wa zamani kuhusu watu wanaowadhalilisha watoto kingono , umemtia mgombea wa chama hicho Jürgen Trittin matatani.

Anashambuliwa na hajui la kufanya. Kwa mshangao huenda akapata kupigiwa kura na wapiga kura ambao ni mara yao ya kwanza kupiga kura. Je chama cha Pirate ama chama chaguo mbadala kwa Ujerumani AfD vitafikia kiwango cha asilimia tano ili kuingia bungeni? SPD kinaelekea kuunda serikali na chama cha kijani na kile cha Die Linke? Hakuna ajuwae kwa hivi sasa . Kuna uwezekano wa aina nyingi.

Mhariri wa gazeti la Frankfurter Allgemeine anazungumzia kuhusu majadiliano ya kuunda serikali baada ya uchaguzi. Mhariri anaandika.

"Itakapotokea kile ambacho hakitarajiwi kutokea katika uchaguzi huu , na kuiweka hali ya kutokuwepo mtazamo halisi wa nadharia, na kulazimika kuleta mvutano baina ya muungano wa vyama vya Christian Democratic CDU na chama cha FDP kwa upande mmoja na Social Democratic SPD na vyama vya mrengo wa shoto vya kijani na Die Linke na hata ikilazimika kuingia madarakani kwa muungano unaoitwa mkuu wa chama cha CDU na SPD kipindi hicho cha utawala kitakuwa wa kihistoria. hata hivyo ni wapiga kura tu ndio wanaoweza kuamua nani anaweza kutawala".

Der Kanzlerkandidat der SPD, Peer Steinbrück, sitzt am 23.04.2013 im Präsidiumssaal im Willy-Brandt-Haus in Berlin und hat Kinder im Rahmen des Türkischen Kindertages eingeladen. Später will der Politiker sich in einem Statement zu der Steueraffäre um den Fußball-Manager Uli Hoeneß äußern. Foto: Wolfgang Kumm/dpa
Mgombea wa chama cha SPD Peer SteinbrückPicha: picture-alliance/dpa

Silaha za sumu

Kuhusu mzozo wa silaha za sumu nchini Syria , gazeti la Stuttgarter Nachrichten linaandika.

Katika harakati kubwa tangu kuanguka kwa mataifa ya mkataba wa Warsaw , rais Putin wa Urusi anataka kuyaonesha mataifa ya magharibi mambo mawili. Kwanza: kuwa majeshi yake yanaweza kutunisha misuli yake tena, kitu ambacho kiongozi huyo wa taifa anakitamani sana. Ni jambo la kushangaza kwa wadadisi wa mambo, baada ya Urusi kujiingia kijeshi katika mapigano katika vita vya jimbo la Georgea mwaka 2008 haya yanatokea. Na cha pili, Putin anataka kuuonesha ulimwengu , kuwa mnyama mkali dubu wa Urusi ambaye alikuwa amelala usingizi wa majira ya baridi kwa muda wa miaka 20 sasa yu macho, na anaweza kufanya chochote.

Russian President Vladimir Putin attends the second working session of the G20 Summit at the Constantine Palace in Strelna near St. Petersburg, September 6, 2013. REUTERS/Dimitar Dilkoff/Pool (RUSSIA - Tags: POLITICS BUSINESS)
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Reuters

Miaka 40 katika Umoja wa Mataifa

Gazeti la Leipziger Volkszeitung linazungumzia kuhusu miaka 40 ya Ujerumani tangu kuingia katika Umoja wa Mataifa.

"Ujerumani sasa ni mwanachama mshiriki wa Umoja wa Mataifa, lakini jamii ya kimataifa bado haijaweza kwa kiasi kikubwa kushughulikia masuala muhimu. Kwa kuwa na wamachama 193 hili halishangazi, hususan katika suala la mzozo wa Syria , sio tu kwa Umoja wa Mataifa, lakini hata kwa upande wa Umoja wa Ulaya limekuwa si jambo rahisi, kuweza kupata msimamo wa pamoja. Hii inaonekana katika baraza la usalama ambapo kuna mvutano wa kuwania madaraka kama ilivyokuwa baada ya vita vikuu vya pili vya dunia".

Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse

Mhariri : Josephat Charo