1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampuni ya Ulaya EADS yapewa kandarasi kubwa na Marekani

1 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DGEa

WASHINGTON:

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetoa kandarasi yenye thamani ya Dola bilioni 35 kwa kampuni ya Ulaya EADS na ya Kimarekani Northrop Grumman kutengeneza madege 179 ya kivita.Hii ni kandarasi kubwa kabisakupata kutolewa na wizara ya ulinzi ya Marekani kwa kampuni ya Ulaya na ni pigo kwa kampuni ya Kimarekani ya Boeing ambayo tangu takriban miaka 50 iliyopita ilikuwa ikidhibiti utengenezaji wa ndege maalum za jeshi la anga la Marekani.