1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampuni ya Volkswagen yafungua kiwanda chake Rwanda

Lilian Mtono
27 Juni 2018

Kampuni hiyo ya Ujerumani imesema hadi magari 5,000 yataunganishwa kwenye kiwanda hicho kipya na cha Kwanza nchini Rwanda

https://p.dw.com/p/30PeL
Ruandas Präsident Paul Kagame bei Einweihung von VW-Werk in Kigali
Picha: Reuters/J. Bizimana

Kampuni ya magari aina ya Volkswagen imefungua kiwanda chake cha kwanza cha kuunganisha magari nchini Rwanda, pamoja na programu ya kompyuta ya ride-sharing ambayo kulingana na kampuni hiyo itafaa kizazi cha vijana wa taifa hilo wanaotumia zaidi teknolojia.

Kampuni hiyo ya Ujerumani imesema hadi magari 5,000 yataunganishwa  kwenye kiwanda hicho kipya, na kutengeneza hadi ajira 1,000, pamoja na kutimiza lengo lake la muda mrefu la kuwa msitari wa mbele katika sekta ya viwanda vya magari inayoinukia barani Afrika.

Mkurugenzi mtendaji wa Volkswagen nchini Afrika Kusini, Thomas Schafer ameisifu Rwanda kwa kuwa na uwezo mkubwa akisema ni nchi iliyojaa vijana wenye mtazamo wa kisasa na inakiu ya kuwa na kiwanda chake yenyewe. Volkswagen tayari imejikita katika baadhi ya nchi barani Afrika, ambazo ni pamoja na Nigeria, Afrika Kusini na Kenya.