1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KANDAHAR: Bomu lauwa watu 6 kusini mwa Afghanistan

13 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3H

Watu 6 wameuawa katika mripuko wa gari lililokuwa na bomu katika mkoa wa kusini wa Kandahar nchini Afghanistani. Watu wengine watano wamejeruhiwa. Lengo dhamira la shambulio hilo lilikuwa msafara wa magari ya majeshi ya kigeni yalioko katika nchi hiyo. Watu 200 wameshauawa mwaka huu katika miripuko ya mabomu katika maeneo ya kusini na mashariki tu ya nchi hiyo.