1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Merkel akabiliwa na mtihani wa kisiasa bungeni leo

29 Septemba 2011

Bunge la Ujerumani leo linapigia kura mfuko wa uokozi katika eneo linalotumia sarafu ya euro. Upinzani unatarajiwa kutoka kwa washirika wa kansela Merkel.

https://p.dw.com/p/12ikf
Kansela wa Ujerumani, Angela MerkelPicha: AP

Kansela wa ujerumani, Angela Merkel, anakabiliwa na mtihani wa kisiasa leo wakati bunge litakapoupiga kura mfuko maalum wa fedha unaolenga kuzisaidia nchi zinazokabiliwa na madeni katika kanda inayotumai sarafu ya euro. Wabunge wa vyama vinavyounda serikali yake ya mseto walio na wasiwasi kuhusu Ujerumani kuisaidia Ugiriki kuondokana na tatizo la madeni, huenda wakapiga kura kuupinga mfuko huo wa thamani ya euro bilioni 440.

Kura za wabunge wa upinzani wanaounga mkono zitahakikisha Ujerumani inaridhia mfuko huo wa uokozi. Finland iliidhinisha kuongeza mchango wake katika mfuko huo hapo jana.