1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Merkel akutana na Rais Putin

Mohamed Dahman8 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DL8m

MOSCOW

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani anakutana na Rais Vladimir Putin wa Urusi kwa mazungumzo yanayotazamiwa kujumuisha suala la ushirikiano wa nishati ,uhuru wa Kosovo na mpango wa nuklea wa Iran.

Maafisa wa serikali ya Ujerumani wamesema suala la uchaguzi wa urais wa wiki iliopita nchini Urusi pia linatarajiwa kujitokeza kwenye mazungumzo hayo yanayofanyika kwenye shamba la rais nje ya mji mkuu wa Moscow.

Kansela huyo wa Ujerumani baadae anatazamiwa kukutana na Rais mteule Dmitry Medvedev ambaye amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa kuchukuwa nafasi ya Putin.

Merkel atakuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kumtembelea Medvedev tokea kufanyika kwa uchaguzi huo ambao makundi ya upinzani na waangalizi wa uchaguzi wa kujitegemea wamesema ulisimamiwa na kudhibitiwa na Ikulu ya Urusi.