1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KARACHI : Bhutto anarudi Pakistan leo

18 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Eq

Wananchi wa Pakistan leo wanasubiri kwa hamu kurudi kwa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Benazir Bhutto baada ya kuishi uhamishoni kwa hiari kwa miaka minane.

Bhutto amekuwa akiahidi kwa miaka kadhaa kurudi nyumbani kukomesha utawala wa kijeshi wa Rais Pervez Musharraf. Lakini inaaaminika kwamba Marekani imekuwa ikishaajisha kwa siri ushirikiano kati ya Musharraf na Bhutto ili kulifanya taifa hilo la Pakistan lenye uwezo wa silaha za nuklea kuwa na msimamo wa wastani na kupendelea mataifa ya magharibi.

Vikosi vya wanajeshi 2,500 wa kupambana na ghasia vimewekwa karibu na uwanja wa ndege wa Karachi na wengine 10,000 wamewekwa katika hali ya tahadhari.

Kurejea kwa Bhuttto ambapo anatarajiwa kupokewa na wafuasi 100,000 kumewezekana baada ya Rais Generali Musharraf kumfutia mashtaka ya rushwa yaliokuwa yakimkabili.