1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KARACHI : Ghasia zauwa watu 34

13 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2a

Makundi hasimu ya kisiasa nchini Pakistan yameshambuliana kwa risasi katika mitaa ya Karachi na kusababisha vifo vya watu 34 na kujeruhi wengine 120.

Hakimu Mkuu Iftikhar Muhammad Chaudhry aliesitishwa kazi hapo mwezi wa Marchi na Rais Pervez Musharraf alisafiri kwenda kwenye mji wa Karachi kuhutubia mkutano wa hadhara lakini ghasia hizo zilimzuwiya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Karachi na hiyo kufuta mpango wake huo.

Makundi ya upinzani yamewalaumu wafuasi wa Musharraf kwa kuandaa vurugu hizo.Tokea kusitishwa katika wadhifa wake kwa madai ya kutumia vibaya madaraka yake Chaudhry amekuwa shabaha ya upinzani uliozagaa nchini Pakistan dhidi ya serikali ya Musharraf aliechukuwa madaraka kufuatia mapinduzi ya mwaka 1999.

Musharraf amefuta uwezekano wa kutangaza hali ya hatari na ameitaka nchi hiyo kuwa kitu kimoja na idumishe amani.