1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Mafunzo

Karandinga: Jinamizi la Mauaji

Grace Kabogo
1 Machi 2017

Inspekta wa polisi George Cross amezongwa na mauaji ya mhudumu kijana wa kike aliyekatwa viungo vyake. Utambulisho wake bado ni siri.

https://p.dw.com/p/2YQTu
DW Crime Fighters Serienmotiv „One Murder too Many“

Uhalifu huu unaweza kuhusishwa na vitendo vya kishirikina? Anaposhughulikia kisa hicho, polisi huyo kijana bila kujitambua anamruhusu mdogo wake wa kike na binamu yake wa kiume kuendeleza ndoto zao kwenye nchi jirani. Melody na Kodjo wanataka kusoma nje ya nchi. Rafiki mmoja jirani amewaahidi kuwapatia mafunzo, hivyo kusisimua matarajio yao ya baadaye. Baada ya kutosikia kutoka kwao kwa muda mrefu, familia ya vijana hao, inaanza kupata wasiwasi. Wakati George anajaribu kuwasiliana na Melody na Kodjo na kushughulikia kesi ya mauaji, anagundua mtandao hatari wa wahalifu wanaofanya biashara ya binadamu.