1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karandinga: Taarifa Nyingi, Moja ya Kweli

Grace Kabogo
4 Oktoba 2017

Sherehe za kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kituo cha vijana zinagubikwa na mauaji ya kikatili ya Musa Bamafor.

https://p.dw.com/p/2lB3S
Crime Fighters Teil 3 Many Facts one Truth

Kulikoni? Mkandarasi wa ujenzi huo alipigwa vibaya hali iliyosababisha kifo chake kutokana na majeraha makubwa. Jammo na Kayla, wenye umri wa miaka 17 kwa bahati walisikia purukushani hiyo, lakini hawakufanikiwa kuwaona wahusika ni kina nani. Wanataka kufahamu zaidi, hivyo wanaanzisha uchunguzi wao binafsi kwa kushirikiana na rafiki yao Fidelis. Je Bamafor alikuwa kweli fisadi, kama kila mtu anavyosema, na hiyo inaweza kuhusishwa na kifo chake? Wapelelezi vijana wanaofanya kazi hiyo bila malipo, wanapata taarifa za kushangaza, ambazo zinabainisha kuwa sio kila taarifa inayoenezwa inaweza kuaminika. Wanagundua njama katika mtandao ambao taarifa za uwongo zimechangia pakubwa.