1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Mafunzo

Karandinga: Unyakuzi wa Ardhi ya Chongwe

Grace Kabogo
1 Machi 2017

Chifu Awombo amekufa, mwili wake ukiwa katika ukingo wa mto katika shamba la maua. Je aliuliwa na mnyama wa mwituni kama serikali inavyotaka watu wa Chongwe waamini? Ama aliuawa?

https://p.dw.com/p/2XcYi
09.2015 Crime Fighters Land of Chongwe (Serienmotiv)

Wengi wanashuku hivyo kwa kuwa shamba la maua ya waridi liko katika ardhi iliyokuwa ikimilikiwa zamani na Chifu Awombo. Inspekta Mwamto anakabiliwa na wakati mgumu kuamua iwapo ashikilie msimamo rasmi au azma yake ya kutafuta hasa kilichotokea. Ni afisa upelelezi Mweri ambaye hatimaye anaanza kuutafuta ukweli. Anagundua suala la ardhi ni gumu mno kuliko lilivyoonekana awali. Linarudi nyuma wakati wa enzi za uhuru na nyaraka haziko katika orodha sahihi. Kuna sio tu kugombania manufaa ya kiuchumi, bali pia hali iliyojaa hisia nyingi. Je, Mweri anaweza kutegua kitendawili cha kifo cha Chifu Awombo? Fuatilia mchezo huu kuanzia mwanzo hadi mwisho wake.