1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katiba ya Umoja wa Ulaya

14 Desemba 2007

Viongozi wa dola na serikali wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya walitia saini jana Lisbon m kataba mpya.

https://p.dw.com/p/CbcB

Katika sherehe maalumu mjiniLisbon,Ureno, jana viongozi wa dola na serikali wa nchi zanachama wa Umoja wa Ulaya walitia saini“ mkataba wa Lisbon“ unaoweka masharti ya kimsingi ya mageuizi ya umoja huo.

„Hilo ni Jiwe la msingi la kuunda Ulaya ya ki-mamboleo na ya kidemokrasi“ –alisema Jose Socrates,Rais wa Ureno-mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya.

Mkataba huu unatazamiwa kuanza kazi 2009 kwa sharti kwamba,nchi zote 27 za-nachama wa Umoja wa Ulaya zimeuidhinisha.

Matamshi waliotoa viongozi hao wa kisiasa yamewahi kusikika kabla na yanajulikana:Ilikua siku ya kihistoria,ukurasa mpya umefunguliwa na msukosuko umeepukwa“-maneno yote hayo yalikwishatumika kabla wakati wa kutiwa saini mikataba ya UU miaka 3 iliopita mjini Roma.Huko katiba ya UU ilitiwa saini na viongozi wa dola 25 zanachama na hali ikawa hivyo jana mjini Lisbon.Lakini ilipokuja kuuidhimnisha mkataba ule kupitia kura ya maoni ya wananchi, ulitiwa munda tangu nchini Ufaransa hata Holland.

Baadae nchi 2 nyengine 2 zikagundua kosa lao la kuutia saini na zikarudi nyuma-nazo ni Uingereza na Poland.

Katika kipindi cha miaka 2 cha majadiliano motomoto ulikuja kuzaliwa mkataba huu mpya wa UU kuchukua nafasi ya katiba iliotiwa munda.

Iliosalia sasa ni kutumai kuwa mkataba huu hautakumbwa na hatima sawa na ile ya katiba ya UU .

Mkataba wa mageuzi kama alivyouita kanzela Angela Merkel wa Ujerumani wakati wa kipindi chake cha nusu ya kwanza ya mwaka huu akiwa rais wa UU, unapaswa sasa kuidhinishwa na wanachama wote 27 tena mnamo muda wa miaka 2 ijayo.

Hivi sasa yadhihirika kana kwamba , ni huko Uingereza tu ambako yamkini kukazuka matatizo.Kwani, wakosoaji wa Umoja wa Ulaya huko wanadai kwa nguvu sana kura ya maoni ipigwe juu ya mkataba huu mpya.

Waziri mkuu Gordon Brown anapanga kuzuwia kura kama hiyo ya maoni,kwavile anajua wazi ,wananchi wenzake wa Uingereza hawautaki mkataba huo.

Wanahofia kuwa na dola kubwa la Ulaya linaloweza kuwabana –Super State- ambalo kwa kuuidhinisha mkataba huo laweza likaundwa.

Ukweli wa mambo ni kuwa, kila nchi mwanachama licha ya mkataba huu, itadumisha bendera yake ya taifa na wimbo wake wa taifa.

Mabishano yasiokwisha ndani ya Umoja huu wa Ulaya kati ya wale wanaopigania mafungamano zaidi na wale wanaon’gan’gania utaifa hayakumalizika.Hata kwa mkataba huu mpya wa Lisbon ingawa ni hatua kweli ya kihistoria iliochukuliwa jana lakini si paa la mwisho juu ya jumba hili.

UU sawa na ulivyokua miaka 50 iliopita utaendelea kupiga hatua mbeler na kupanuka ,baadhi ya wakati pole pole na baadhi ya nyakati kwa kasi.

Mkataba wa Lisbon,si wa mwisho.Kama kifuta machozi kwa wale wote waliokuwa na shaka shaka:kwa mara ya kwanza kabisa mkataba wa Umoja wa Ulaya unatoa uwezekano kwa mwanachama yeyote kujitoa kutoka Umoja huu akitaka na sio ni pingu za maisha.