1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ba Ki Moon, miezi sita tangu kukamata madaraka

11 Julai 2007

Katika ofisi za makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York watu watu wanano’gona juu ya hali ya babade ya katibu mkuu, Ban Ki Moon. Mwananchi huyo wa Korea Kusini analaumiwa kwamba anaonekana sio meneja mzuri, yu karibu mno na serekali ya Marekani na anazungumza vibaya lugha ya Kiengereza kuweza kuwasiliana vizuri na watu katika masuala ya kiufundi.

https://p.dw.com/p/CHB5
Ban Ki Moon, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Ban Ki Moon, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.Picha: AP Graphics

Miezi sita imepita tangu Ban Ki Moon aingie madarakani, lakini yaonesha ustahamilifu unaanza kupungua; na suala ni juu ya mustakbali wake:

+Mimi ninachoona nini kinachofanywa na Ban Ki Moon na utawala wake ni kama mahala pa ujenzi.+

Sio tu huyo bingwa wa masuala ya Umoja wa Mataifa kutoka Chuo Kikuu cha Columbia, Edward Luck, anayeiona ofisi ya mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa ni mahala kama pa ujenzi. Zaidi ni kwamba imechukuwa muda mrefu kwa waziri huyo wa zamani wa mambo ya kigeni wa Korea Kusini kuuzowea wadhifa wake, imemchukuwa muda mrefu mno, wanadai wahakiki wengi.

+ Watu wengi wanalaumu mtindo wake wa kuendesha mambo au uwezo wake wa kuwasiliana na watu pale anapoelezea suala fulani.+

Tusisahau namna alivojikwaa kuhusu suala la adhabu ya kifo na namna alivoisifu Marekani katika kile alichokiita kuleta utulivu katika Iraq. Mtizamo wa Ban Ki Moon umekuwa mara kadhaa karibu na ule wa Ikulu ya Marekani.

+ Mtu ana hisia kwamba Ba Ki Moon anajiamini anavoingiliana an Marekani.+

Lakini pia marafiki zake wa Kimarekani wameshangazwa nae kuhusu masuala ambayo anayapa kipa umbele au maamuzi yake kuhusu kuajiriwa maafisa wa umoja huo.

Kwa mujibu wa Bwana Luck ni kwamba mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ana mtindo wa kujizungusha na watu anaowapenda, na katika hali fulani amejichagulia watu walio sawa kwake, lakini wamepewa dhamana; na ukiangalia uzoefu wao ni jambo lisiloingia akilini. Malalamiko ndani ya kumbi za makao makuu ya Umoja wa Mataifa na hata miongoni mwa mabalozi wa nchi za Magharibi na nchi zisizoelemea upande wowote yamehanikiza kutaka Ban Ki Moon abadilishwe.

Ban Ki Moon, katika kulinda heshima, anaweza kuwa rais wa nchi yake. Lakini katika kampeni za uchaguzi za nchi hiyo, katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa hana nafasi kabisa; na haya ndio makisio ya mwandishi wa televisheni ya Kijerumani, ARD, Martin Fritz. Hata hivyo angalau kwa wale wanaomuunga mkono huko N ew York, kama vile baloziwa Uchina Wang, ni kwamba uchapaji kazi wa Ban Ki Moon utaboreka.

+Amejitahidi kwa uwezo wake wote. Bila ya shaka yeye ni mtu mpya katika Umoja wa Mataifa, hajakulia katika umoja huo, kwa hivyo tufanye haki kwa kumpa wakati wa kujifunza.+

Lakini kuna watu wengine wanaovutiwa naye. Marafiki zake wanamsifu kwa ukakamavu wake na ari ya kukabiliana uso kwa uso na matatizo makubwa kama vile yale ya Mashariki ya Kati na Darfur. Hajuwi kusema SIO. Wahakiki wanasema hafanyi vya kutosha kugawa madaraka, na hata akiweko mjini New York hujifungia ofisini na washauri wake. Tena Bwana Luck:

+Hatutaki kuwa na mfalme wa falsafa kama katibu mkuu, lakini tunahitaji mtu anayeweza kuwasiliana na umma na mtu ambaye anaaminiwa na nchi wanachama, na katika jambo hilo sisi hatujafikia.+

Nguvu ya kauli ndio uwezo aliokuwa nao mtangulizi wa Ba Ki Moon. Na hii haitokani tu na upungufu wa Mkorea huyo katika kuitamalaki lugha.