1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kauli za chuki katika kandanda la Ujerumani

Bruce Amani
4 Januari 2018

Jinsi ya kukabiliana na hotuba za chuki zinazotokana makundi au watu wa misimamo mikali kwenye majukwaa ya intaneti kimekuwa shughuli ya kila siku kwa vilabu vya kandanda vya Ujerumani

https://p.dw.com/p/2qL07
Fussball - Eintracht Frankfurt Präsident Peter Fischer
Picha: picture alliance/dpa/A. Arnold

Vilabu vya Bundesliga vinaendelea kulengwa kupitia kauli za chuki za siasa za mrengo wa kulia kwenye mitandao ya kijamii, na hali sasa imeongezeka katika klabu ya Frankfurt.

Chama cha AfD cha mjini Frankfurt katika jimbo la Hesse kimewasilisha kesi ya kuchafuliwa jina dhidi ya rais wa Eintracht Frankfurt  Peter Fischer baada ya kusema kwenye mahojiano aliyofanya na vyombo vya habari akisema kuwa waiga kura wa AfD hawnaa nafasi katika klabu hiyo.

Fischer ambaye anasisitiza kuwa michezo lazima iwe ya kisiasa, ameapa kuzungumzia suala hilo katika mkutano wa kila mwaka wa klabu hiyo mnamo Januari 28 wakati maafisa wa AfD wametuma maombi ya uwanachama katika klabu hiyo kama hatua ya kupinga msimamo wa klabu hiyo.

Hannover AfD Parteitag Nationalhymne
Viongozi wa siasa kali za mrengo wa kulia wa AfD Picha: picture-alliance/dpa/J. Stratenschulte

Kesi hiyo huenda sasa ikaenda mahakamani, na mwanachama wa bodi ya Frankfurt Axel Hellmann ameliambia gazeti la Bild kuwa klabu hiyo mara nyingine huwaajiri watu sita au saba ambao hufuta kwenye mitandao yao ya kijamii ujumbe mbaya, hasa unaowalenga wageni.

Frankfurt, sio klabu pekee inayolengwa na ujumbe wa kibaguzi na kuwachukia wageni. Msemaji wa Freiburg amesema "ujumbe wa matusi lazima ufutwe” haraka iwezekanavyo kwenye majukwaa yao ya intanet wakati kocha wao Christian Streich anapotoa kauli za kuwaunga mkono wakimbizi.

Msemaji wa Bayer Leverkusen Dirk Mesch pia alisema kukabiliana na kauli za kibaguzi na kuwachukia wageni kimekuwa kitu cha kawaida.

Ujerumani ilianzisha sharia ya kupambana na hotuba za chuki mnamo Januari mosi ambayo inaihitaji mitadao kama vile Facebook, Twitter na YouTube kuondoa ujumbe ambao unakwenda kinyume cha sharia ndani ya masaa 24 baada ya kuripotiwa, la sivyo itozwe faini kubwa.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA
Mhariri: Daniel Gakuba