1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Changamoto zinazomkabili Rais Mteule Uhuru Kenyatta

1 Aprili 2013

Rais Mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta wakati huu anatazamwa kama kiongozi anayekabiliwa na changamoto kadhaa katika uundaji wa serikali yake.

https://p.dw.com/p/187d1
Rais Mteule Uhuru Kenyatta wa Kenya
Rais Mteule Uhuru Kenyatta wa KenyaPicha: Reuters

Hayo yametokea baada ya hapo Jumamosi, Mahakama ya Juu ya nchi hiyo kuamua kuwa yeye ndiye mshindi halali wa kiti cha urais wa taifa hilo na kulitupilia pingamizi la mpinzani wake Raila Odinga. Kutoka mjini Nairobi Sudi Mnette amezungumza na mchambuzi wa siasa za Kenya, Profesa Chacha Nyaigoti Chacha, kuhusiana na matarajio ya serikali mpya ya Kenya chini ya Uhuru Kenyatta. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri: Mohammed Khelef