1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya imemrejesha Sheikh Abdulla Al-Faisal nchini Jamaica

21 Januari 2010

Serikali ya Kenya imemrejesha nchini kwao Mhubiri kutoka Jamaica Sheikh Abdulla Al-Faisal ambaye amekuwa kizuizini kwa muda wa zaidi ya wiki mbili.

https://p.dw.com/p/LdBc

Abdulla Al- Faisal ambaye kuzuiliwa kwake kuliepelekea jamii ya waislam kufanya maandamano yaliyosababisha vifo vya watu wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa wakiwemo maafisa wa usalama alitarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni baada ya wanaharakati wa haki za binadamu kuteta kwamba kuzuiliwa kwake ni kinyume cha sheria kwani alikuwa na stakabadhi za kuwa nchini Kenya.

Wakati huo huo, Msemaji wa serikali Dr. Alfred Mutua amekiri kwamba wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab waliodaiwa kushiriki kwenye maandamano ya siku ya Ijumaa wametisha kuivamia Kenya.

Kutoka Nairobi Mwandishi wetu Alfred Kiti ametuandalia taarifa ifuatayo.