1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya inatafuta nishati ya maji ya moto chini ya ardhi

Miraji Othman26 Novemba 2009

Ukame unaifanya Kenya itafute nishati mbadala

https://p.dw.com/p/KgJD
Ukame umetanda nchini Kenya. Karibu na Mto Athi, ng'ombe amekufa karibu na machinjo cha Shirika la Nyama la Kenya, KMC.Picha: picture alliance / dpa

Kenya inahitaji dola bilioni 1.02 mnamo miaka mitatu ijayo ili iweze kutumia uwezo wake wa kutoa umeme kutokana na nguvu za maji ya chini ya ardhi. Nishati hiyo inaonekana kuwa ni jibu la kuachana na kutegemea sana nguvu za umeme unaotokana na nguvu za maji ya mito ambayo inakumbwa na ukame. Hayo yameelezwa na waziri wa nishati wa nchi hiyo, Kiraitu Murungi. .

Ukame umepunguza maji katika mabwa akubwa ya maji huko Kenya, hivyo kusababisha umeme kukatwa kila wakati na kupelekea kutegemea majenereta yanayofanya kazi kwa mafuta ya diseli. Hali hiyo imefanya bili za umeme kwa wateja kupanda juu.

Uchumi mkubwa wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki umekuwa ukitegemea umeme unaotokana na nguvu za maji ya mito kwa asilimia 90, na nchi hiyo inatoa Megawatt 1,300 za umeme wa aina hiyo. Hivi sasa uchumi wa nchi hiyo unahitaji kuengeza Megawatt 1,800 katika gredi lake ili kutosheleza  mahitaji mepya. Karibu ya Megawatt 200 hivi sasa zinatoka kwenye nishati ya maji ya chini ya ardhi, japokuwa serekali inakisia kwamba kuna uwezekano wa kutoa Megawatt 7,000

Waziri Murungi aliuambia mkutano kwamba kampuni ya kuendeleza nishati ya maji yanayotoka chini ya ardhi itahitaji karibu magredi 12 ifikapo mwaka 2010 hadi 2011 ili kuchimba visima 72 kila mwaka, na kupata majenereta mia moja mnamo miaka mitatu ijayo. Fedha zinazozohitajiwa ni pamoja na dola milioni 324 kwa kupata magredi hayo na dola milioni 700 kwa majenereta. Alisema kampuni hiyo ya nishati ya maji moto kutoka chini ya ardhi pamoja na kampuni ya umeme ya Kenya, KenGen, zimepata fedha na zimetoa kandarasi kwa ajili ya magredi mawili, na zinatafuta fedha kwa ajili ya magredi mengine mawili.

Waziri Murungi alisema kizingiti kikubwa katika kuwekeza katika nishati inayotokana na maji ya chini ya ardhi ni gharama kubwa zinazohitajika. Kwa mfano, zinahitajika dola milioni 6.2 hadi 6.5 kuchimba kisima, na jenereta linagharimu baina ya dola milioni saba na nane. Alisema imekuwa vigumu kuwavutia wawekezaji wa kibinafsi katika sekta ya nishati ya maji ya kutoka chini ya ardhi kwa sababu ya gharama kubwa za mwanzoni. Hata hivyo, alitaja kwamba Kenya inahitaji kuengeza uzalishaji wa nishati ili kutosheleza mahitaji yanayoongezeka.

Pia nchi hiyo inataka kupanua utaoaji wa nishati kutoka kwenye viini vingine. Hiyo ni pamoja na kupata Megawatt 300 kutoka upepo, ambapo kampuni juu ya jambo hilo huko kaskazini mashariki ya Kenya itaanza kutoa nisahti hiyo mwaka 2012. Serekali inasema kuna uwezekano wa kupata Megawatt 2,000 za umeme kutoka upepo.
Kenya imetumia dola milioni 8.43 mnamo miaka minne iliopita kwa ajili ya kulipia umeme unaotokana na nguvu za juwa katika mahospitali, shule na vituo vya afya, na imetenga shilingi milioni 500 nyingine kwenye bajeti ya  mwaka 2009 na 2010. 

Mwandishi:  Miraji Othman/Reuters

Mhariri:  Mohammed Abdulrahman