1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Maandamano yaliyopangwa kufanyika leo hii yamezuiliwa

17 Februari 2010

Nchini Kenya serikali imetoa ahadi kwa waliotaka kuandamana kuwa malalamiko yao yatashughulikiwa.

https://p.dw.com/p/M3j9
Ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi mwaka 2007 nchini Kenya.Picha: AP

Maandamano yaliyopangwa kufanyika leo Kutokea mkoa wa Bonde la Ufa nchini Kenya hadi mjini Nairobi na Wakenya Takriban elfu kumi ambao walipoteza makazi yao katika mapigano ya kikabila yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Desemba mwaka juzi, yamesitishwa, baada ya waandamanaji hao kupewa ahadi na serikali kuwa malalamiko yao yatashughulikiwa.

Awali Serikali ya Rais Mwai kibaki iliahidi kuwalipa fidia Wakenya hao waliopoteza makazi yao kutokana na mzozo wa kikabila uliozuka baada ya uchaguzi huo mkuu wa Kenya, lakini bado haijatimiza ahadi hizo.

Halima Nyanza alizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Bonde la Ufa, Amos Gacheca, kuhusiana na kile kilichosababisha hatimaye kusitishwa kwa maandamano hayo yaliyoanza jana katika jimbo hilo la Bonde la Ufa.

Mahojiano/Halima Nyanza

Mpitiaji:Abdul-Rahman,Mohammed