1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Mabilionea 40 na ombaomba milioni 40

Amina Mjahid
9 Januari 2018

Japokuwa Kenya inamulikwa katika vyombo mbali mbali vya habari kama taifa lililogawika kwa misingi ya kikabila, kihalisia inayo makabila mawili tu - matajiri na masikini. Ukabila ni ziada tu ya hali ngumu wanayopitia.

https://p.dw.com/p/2qaSO
DW - eco@africa: Plastikmüllverarbeitung zu synthetischem Öl
Picha: DW

Katika miezi ya hivi karibuni siasa za urais ndiyo zilihanikiza katika vyombo vya habari vya kimataifa kuhusiana na taifa hili la Kenya. Mahasimu wa kisiasa rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga ambao ni watoto wa rais wa kwanza na makamu wa rais wa kwanza wa taifa hilo la Afrika Mashariki, wamewania nafasi hiyo ya juu kabisaa katika mazingira yaliozingiwa na mapambano ya kisheria, rushwa na vurugu zilizofadhiliwa na serikali.

Mnamo Agosti 8 matokeo ya uchaguzi wa awali yalipelekea tukio la kwanza la kufutwa kwa uchaguzi na mahakama katika historia ya bara la Afrika. Lakini hata baada ya uchaguzi mpya uliyomrejesha Uhuru Kenyatta kufanyika, huku ukisusiwa na wananchi wengi, bado hali ya kisiasa haijatulia.

Kenia Uhuru Kenyatta  William Ruto
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wakiteta jambo.Picha: Getty Images/AFP/T. Karumba

Miaka kumi  iliyopita Raila Odinga na Uhuru Kenyatta waliwania kiti cha urais katika uchaguzi mwingine uliobishaniwa, wakati huo ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008 zilisababisha mauaji ya zaidi ya watu 1200 huku wengine zaidi ya laki sita wakipoteza makaazi yao, kwa uhakika waandishi habari wa upande wa Magharibi mwa nchi hiyo waliandika na kusema ukabila ndio kitu kinachoigawanya nchi kisiasa. 

Waathirika wakubwa ni raia masikini

Wakati ukabila unatoa mchangao katika kuchochea wasiwasi kipindi cha uchaguzi, hauwezi kuwa kielelezo cha nyufa za kisiasa zinazolikumba taifa hilo.  Waathirika wa ukosefu wa usawa nchini Kenya hawatoki kwenya kabila moja au kundi la kimkoa. Ni wananchi masikini waliyo katika maeneo ya mijini na mashambani. Na kutwezwa kwao, ambako ni matokeo ya rushwa iliokithiri, ukandamizaji na maendeleo yanayozingatia kanuni za kibepari - kutaendelea kuchochea moto wa kisiasa.

Katika taifa hilo ambako viongozi wa kisiasa wanajulikana kwa magari ya kifahari wanayomiliki, huku karibu asilimia arobaini ya idadi ya watu nchini Kenya wakiishi chini ya kiwango cha umasikini, wakenya wanatambua kuwa japokuwa hawazungumzi lugha moja na hawafuati dini moja, wanakabiliwa na tatizo la pamoja la ukosefu wa usawa.

Raila Odinga
Kiongozi wa upinzani na kinara wa muungano wa NASA Raila OdingaPicha: Getty Images/AFP/Y. Chiba

Katika Juhudi ya kulitatua hili mwanaharakati aliegeuka mwanasiasa Boniface Mwangi, alisisitiza ushirikishwaji wa kisiasa, na kulaani rushwa ya kisiasa wakati akiwania kiti cha ubunge. Akiwakilisha sauti kubwa lakini iliotengwa ya wapinzani, aliwambia wapigakura kuwa: "Nina habari kwenu kwamba, Kenya ina makabila mawili tu - maskini na matajiri. Habari njema ni kwamba wimbi linabadilika." Hata hivyo Wakenya wamekwisha iona filamu hii hapo kabla.

Ukosefu wa usawa na rushwa vilichukuwa nafasi kubwa katika mijadala ya kisiasa katika miaka ya 1970, na pia mijadala kuhusu ukomo wa mamlaka ya rais, rushwa katika taasisi na ugatuzi wa rasilimali za serikali viliamsha mijadala kuhusu ukosefu wa usawa. Wafausi wa Odinga walidai kuwa Kenya sasa imegueka taifa la Mabilionea 40 na ombaomba milioni 40.

Licha ya vyombo vya habari kuangazia zaidi sula la ukabila, mfanyakazi wa wastani nchini Kenya anapokea kiasi cha dola 150 kwa mwezi, wakati mbunge anapokea karibu mara 50 ya kiwango hicho. Siasa za uchaguzi zinaendelea kuwa njia kuu ya kujipatia uatjiri na madaraka, na Wakenya wa kawaida wanajua fika kuwa hawapati chochote.

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Iddi Ssessanga