1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Nafasi kwa wawekezaji wa Ujerumani

27 Septemba 2012

Uchumi wa Kenya unakua,na hali hii imekuwa ikiendelea kwa karibu miaka kadha sasa. Hususan sekta ya teknolojia,hivi sasa inakua kwa kasi kubwa, ikiwa na maendeleo mapya kwa upande wa simu za kisasa za mkononi .

https://p.dw.com/p/16Fsz
nairobi 014 © vladimir kondrachov #496811
Mji mkuu wa Kenya NairobiPicha: Fotolia/vladimir kondrachov

Hali  hii  inawavutia  wawekezaji  wa  kimataifa. Hata hivyo wafanyabiashara  wa  Ujerumani  hadi  sasa  wamekuwa wakijizuwia  kuingia  katika  soko  hili. Lakini  hali  hiyo  inakaribia kufika  mwisho, kwa  kuwa  katika  mji  mkuu  Nairobi linafanyika jukwaa  la  kiuchumi  kati  ya  Ujerumani  na  Kenya  linaloanza  hii leo (26.09  hadi Novemba  28).

Wakati   ukizungumzia  kuhusu  uwekezaji  nchini  Kenya ,si  kwamba unaizungumzia  tu Kenya  pekee  yake. Kwasababu  nchi  hiyo ni  njia  ya  kuingia  wawekezaji  kutoka  nje  kwa  eneo  lote  la Afrika  mashariki. Nchi  hiyo ina   bandari  katika mji wa  Mombasa  na  bandari  hii  haitumiki  tu  na  nchi  ya  Kenya  yenyewe  binafsi ,  bali  pia  kwa mataifa  jirani ambayo  bidhaa  zake  zinasafirishwa  kwa  meli.

Hata  maendeleo  yaliyopigwa  na  uongozi  wa  nchi  hiyo  na uwekezaji  katika  miundo  mbinu  yanawavutia  wawekezaji.

Wer hat das Bild gemacht/Fotograf?: Alfred Kiti (DW-Korrespondent) Wann wurde das Bild gemacht?: 22.08.2012 Wo wurde das Bild aufgenommen?: Nairobi, Kenia Bildbeschreibung: Bei welcher Gelegenheit / in welcher Situation wurde das Bild aufgenommen? Wer oder was ist auf dem Bild zu sehen? Das Displays des Handys zeigt die Anwendung M-Pesa, auf der gerade Geld aufgeladen wurde. M-Pesa ist eine Anwendung, mit der Mobiltelefonnutzer Geld in Form von Gesprächsguthaben überweisen können.
Teknolojia ya simu za mkononi ilivyppiga hatua nchini KenyaPicha: DW

Hata  hivyo  wafanyabiashara  wa  Ujerumani  hadi  sasa wamekuwa  wakijizuwia  kuwekeza  nchini  humo. Lakini  sasa chama  cha  wenyeviwanda  nchini  Ujerumani  na  wafanyabiashara wameanzisha  ofisi  maalum  mjini  Nairobi. Ingo Badoreck anawakilishi  maslahi ya   kiuchumi  ya  Ujerumani  nchini  humo. Kwake  yeye  anasema  uwezo  wa  Kenya  haujawekwa  katika  hali halisi.

"Tumepata  ukuaji  mkubwa  hapa  nchini  Kenya,  hali  ambayo haijatambuliwa  na  uchumi  wa  Ujerumani. Hapa  tuna  miradi mikubwa  ya  miundo  mbinu  na  pia  katika  sekta  ya  afya, katika sekta  nishati  inayoweza  kutumika  tena, na  hii  ni  miraji  ambayo inapendelewa  pia  na  wawezekaji  wa  kati".

ARCHIV - Der Frachter Hansa Stavanger kommt am 8. Aug. 2009 am Hafen von Mombasa, Kenia, an. Der Kapitaen des gekaperten Frachters, Krzysztof Kotiuk, fordert nach einem Vorabbericht des Nachrichtenmagazins "Focus" von Samstag, 15, Aug. 2009, Schadenersatz von der Hamburger Reederei Leonhardt
Meli ikikaribia katika bandari muhimu ya Mombasa nchini KenyaPicha: Anonymous/AP/dapd

Wafanyabiashara  wakubwa  wa  sekta  ya  nishati  tayari wamekuwa  wakifanyakazi  nchini  Kenya, kama  vile  kampuni  la kemikali  la  BASF,  ambapo  kilimo  na  sekta  ya  ujenzi  vimekuwa sehemu  muhimu  ya  ziada  kwa  makampuni  haya nchini  Kenya. Kampuni linalotengeneza  vipodozi la  Baiersdorf  linazalisha  bidhaa  kwa  ajili ya  soko la  eneo  lote  la  Afrika  mashariki. Hii  imewezekana kutokana  na  idadi  kubwa  ya  wafanyakazi  ambao  wana  elimu  ya kutosha  katika  suala  hilo. Kwa  ukuaji  wa  uchumi  wa   wastani wa  asilimia  tano , nchi  hiyo  imekuwa  injini  muhimu  ya  uchumi  wa Afrika  mashariki.

Drago Buzuk  ana  matumaini  makubwa  zaidi  kwa  mwaka  ujao. Yeye  anawakilisha  kampuni  la  "German Teknology Solutions", ambalo  linajumuisha  makampuni   30  ya  Ujerumani   ya  kiwango cha  kati. Makampuni  yote  hayo  yana  matumaini , kuwa  mataifa ya  Afrika  mashariki  kwa  kuwa   na  utajiri  wa  maliasili  yanaweza kukua  na  kuwa  kama  China  katika  muda  wa  miaka  20  ijayo. Lakini unatokea  pia  ushindani  kutoka  eneo  hilo, anasema  Buzuk.

"Tatizo  ni  kuwa  uchumi  wa  Ujerumani  umetelekeza  eneo  hilo kwa  kiasi  kikubwa  na  hapa  kuna  wafanyabiashara  wachache kutoka  Ujerumani, ambao  wanaweza  kushughulika  na  shughuli  za kawaida  za  kila  siku  na  kuweza  kuongoza  hatua  za maendeleo.Kwa  upande  wa  Wachina  hilo  ni  tofauti. Pia  kuhusu suala  la  upatikanaji  wa  fedha , wanaodhibiti  ni  Wachina ambao wako  haraka  kufanya  hivyo".

BILDAUSSCHNITT: Chancellor of the Federal Republic of Germany Angela Merkel, right, with Kenyan President Mwai Kibaki, middle, at State House Nairobi at a welcoming ceremony on the first day of her two-day official visit to Kenya., Tuesday July 12, 2011. (Foto: Khalil Senosi/AP/dapd)
Rais wa Kenya Mwai KibakiPicha: dapd

Mwakilishi  wa  mambo  ya  uchumi Ingo Badoreck  anapambana  na ushindani  huo  kutoka  Asia  kwa kujiamini.Kwake  yeye  suala  ni kuhamisha  utaalamu.

"Hicho  ndio  kitu  muhimu, ambacho  washirika  wetu  wa  Asia hawakiwezi. Sio  tu  kwamba  tunauza  bidhaa  zetu  hapa   na bidhaa  zetu  kuziingiza  katika  soko  la  Kenya, lakini  tunajaribu  pia kuingiza  utaalamu  na  ujuzi  wetu kwa  watu  wa  hapa".

Tunawezaje  basi  kuchochea uwezo  wa  wafanyabiashara  wa Ujerumani  kuelekea  Afrika? Kazi  hiyo  inafanywa  na  kundi  la chama  kinachohusika  na  Afrika, ambacho  kinapata  fedha  kutoka katika  uchumi  wa  Ujerumani. Lakini  kazi  hiyo  inakuwa  ngumu , anasema  Asman Nitardy  ambaye  anashughulika  na  chama  hicho katika  eneo  la  Afrika  mashariki. Kutokana  na  kazi  yake amesababisha  makampuni  mengi  kujizuwia  kutoa  picha  mbaya ya  Afrika  katika  vyombo  vya  habari.

Mwandishi : Maja Braun /ZR / Sekione  Kitojo

Mhariri: Mohammed  Abdul Rahman