1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi dhidi ya Pistorius yafikia awamu muhimu

5 Mei 2014

Kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius imeanza tena kusikizwa. Kesi hiyo imefikia awamu muhimu wakati mawakili wa Pistorius wakijaribu kujikwamua kutokana na mwanzo mbaya.

https://p.dw.com/p/1Bu6r
Oscar Pistorius Pretoria 8. April
Picha: Reuters

Ilikuwa zamu ya jirani na rafiki aliyesimulia matukio ya kuhuzunisha ya kilichotokea usiku huo nyumbani kwa Pistorius, akisema alimkuta mwanariadha huyo akiteremka ngazi za nyumba yake akiwa amembeba mikononi mchumbake aliyekuwa amefariki.

Baada ya mapuzimko ya wiki mbili, upande wa mshtakiwa ulimuita Johan Stander, aliyekuwa mtu wa kwanza kufika nyumbani kwa Pistorius baada ya mwanariadha huyo kumpiga risasi Reeva Steenkamp mwaka jana.

Stander ameiambia mahakama kuwa alipigiwa simu na Pistorius, aliyemwarifu kuwa amempiga risasi na kumuua Reeva.

Mawakili wa Pistorius watatumia wiki mbili zijazo kujaribu kuuweka pamoja ushahidi wa mwanariadha huyo na kuyapinga madai ya upande wa mashitaka kuwa alimpiga risasi mchumba wake baada ya kutokea ugomvi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman