1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya Fritzl Austria

18 Machi 2009

Mshtakiwa huyo aungama hatia.

https://p.dw.com/p/HF07

Josef Fritzl, baba wa ki-austria anaekabili mashtaka kwa kumfuga na kumbaka mwanawe wakike, Elisabeth kwa miaka 24, katika chumba chini ya ardhi nyumbani kwake, amekiri leo mashtaka yote aliotuhumiwa pamoja na lile la kuua na kumgeuza mwanawe mtumwa.

Baba huyo mwenye umri wa miaka 73 ambae alikwishaungama madhambi ya kulala na mwanawe wakike ,kumfuga i na kumuingilia kwa nguvu kimapenzi ,ghafula na bila kutarajiwa aligeuza ulimi wake alipokataa hapo awali shtaka la kumuua mtoto wao mchanga kupitia dharau.

Josef Fritzl aliiambia leo mahakama huko Austria kuwa yeye ni dhamana ya kifo cha mtoto mchanga Michael aliezaa na mwanawe wa kike, Elizabeth, katika chumba aliechokuwa akimfuga cha chini ya ardhi. Mtoto huyo mchanga Michael ,mmoja kati ya watoto-pacha, alikuwa mgonjwa tangu kuzaliwa hapo 1996 na aliishi kwa masaa 66 tu.

Fritzl, hata hivyo, aliambia Mahakama hakumuachia makusudi mtoto huyo mchanga afariki isipokuwa hakudhania kuwa ni mgonjwa hivyo.

Mzee huyu wa Kiauastria ameungama kuwa hali ambayo alimfuga binti yake ni aina ya handaki lisilo hata na dirisha na ni sawa na kumfanya mtumwa.

Ilikua ushahidi kwa njia ya video alioutoa mwanawe huyo wa kike, Elizabeth, Fritzl aliiambia Mahakama,uliomfanya kuungama madhambi yake ya kusababisha kifo cha mtoto Michael na ya kumfuga mwanawe-mashtaka ambayo hapo kabla alikanusha.

Uvumi wa vyombo vya habari kuwa binti yake Elizabeth alikuwapo binafsi leo mahakamani wakati wa kesi ikisikilizwa haukukanushwa tangu na msemaji wa mahakama hata na wakili Rudolf Mayer.

Shtaka la kuua linaadhibiwa nchini austria kwa kifungo cha maisha, wakati shtaka la kumfanya mtu mtumwa limechomoza kwa mara ya kwanza nchini Austria, na linatoa adhabu ya kifungo cha miaka 20 korokoroni.

Katika siku ya 3 ya kesi hii, mtaalamu wa kiakili ameambia leo Mahkama kwamba Josef Fritz ana akili zake timamu kwa alioyatenda.

Kwa mara ya kwanza leo tangu kuanza kesi yake, Fritzl hakujifunika uso wake, akiingia mahkamani kama alivyokuwa akifanya kabla, akijiziba uso kwa file ya rangi ya buluu. Upande wa mashtaka na ule wa utetezi unatazamiwa kutoa taarifa zao za mwisho kwa jopo la mahakimu hapo kesho. Na hukumu ya mwisho ilioharakishwa sasa kwa kuungama Fritz madhambi yake,inatarajiwa pia kesho kesho.

Muandishi:Ramadhan Ali

Mhariri: O.Miraji