1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya Khodokovsky kuanza kesho

Saumu Ramadhani Yusuf14 Desemba 2010

Hukumu inatazamiwa kutangazwa na mahakama ya Urusi

https://p.dw.com/p/QXbA
Mikhail KhodorkovskyPicha: AP

 Mahakama nchini Urusi inatazamiwa siku ya jumatano kutangaza hukumu yake katika kesi dhidi ya aliyekuwa tajiri mkubwa nchini humo Mikhail Khodorkovsky kesi ambayo inafuatiliziwa kwa karibu kimataifa.Khodorkovsky tayari anatumikia kifungo cha miaka minane kutokana na  kuhusika na udanganyifu.Sasa anakabiliwa na kesi ya kujilimbikizia fedha pamoja na wizi.

Khodorkovsky mkuu wa iliyokuwa kampuni kubwa ya mafuta ya Yukos anakabiliwa hivi sasa na kesi mpya ya kuhusika na wizi pamoja na kujilimbikizia fedha chungunzima na katika kesi hiyo huenda akajikuta akihukumiwa tena miaka 14 jela. Khodorkovsvky anatuhumiwa kuiba tani millioni 218 za mafuta zenye gharama ya dolla billioni 26.Hii ni kesi inayotajwa kuwa ya utata mkubwa nchini Urusi na inayomfanya Khodokovsky kuonekana pia kama shujaa  na wafuasi wake kutokana na kuonekana kama anayeadhibiwa kwa kuthubutu kumpinga waziri mkuu Vladmir Putin. Hata hivyo maafisa nchini humo wanasema kwamba Khodokovsky ni mtu fisadi ambaye amevunja sheria.Hata hivyo wakili wa mtuhumiwa huyo Wadim Kljuwgant anasema kesi hii ambayo ni ya pili itakwenda bila ya kuzingatia haki kwa mteja wake.

 ''Kila kitu ni uongo kila mahala uongo umetapakaa.tangu mwanzo hadi mwisho ni uongo mtupu.Kuanzia neno la mwanzo hadi la mwisho hakuna kilicho kweli.kinachozungumzwa na kinachoandikwa kila kitu kimetungwa kwa lengo moja tu.kulipiza kisasi''

Hata katika nchi za magharibi kesi dhidi ya Khodokovsky na mfanyibiashara mwenzake Platon Lebedjew inatazamwa kwa jicho la kuikosoa.Hata waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle alipokuwa Urusi tarehe mossi Novemba alizungumzia wasiwasi wa Ujerumani kuhusiana na kesi hiyo.Alimwambia mwenzake wa nchi hiyo Sergei Lawrov kwamba wasiwasi huo ni kwa maslahi ya Urusi katika nchi hizo za magharibi.

Ama kwa upande mwingine Oleg Orlow anayefuatilia kwa karibu kesi hiyo nchini Urusi anasema inawezekana mahakama kutoa uamuzi wake katika kesi hiyo kwa kuzingatia uhuru lakini hilo kwa uapnde mwingine linabanwa pia na mahakama hiyo.

'' Orlow

Jaji Danilkin kwa sasa yuko katika hali ngumu ya kufanya uamuzi.Naweza kutafakari ni kwa jinsi gani atabidi kuwa mwangalifu katika uamuzi wake.Lakini nchini Urusi kila kitu kinawezekana''

Kesi dhidi ya Khodokowsky inachukua nafasi muhimu sana katika historia ya Urusi  pamoja na katika jamii ya wafanyibiashara nchini humo.Inasadikiwa kwamba maamuzi juu ya kesi hiyo zaidi hayatatoka mahakamani bali katika ikulu ya Kremlin ambako kuna mitizamo tofauti kuhusu kesi hiyo suala lakini ni mtizamo wa nani utakaozingatiwa kuamua kesi hiyo.

Mwandishi Winogradow Jegor/Saumu Mwasimba

Mhariri AbdulRahman.