1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya maafa ya Duisburg yaanza

Thelma Mwadzaya27 Julai 2010

Waendesha mashtaka wa Ujerumani wameifungua rasmi kesi ya maafa yaliyotokea mwishoni mwa wiki wakati wa tamasha la muziki aina ya Rock,Love Parade.

https://p.dw.com/p/OVK6
Purukushani DuisburgPicha: AP

Kulingana na msemaji wa afisi ya mwendesha mashtaka,mahakama itatathmini mbinu zilizotumika kuwaruhusu watu zaidi ya milioni moja kushiriki katika tamasha hilo kinyume na idadi ya laki mbili u nusu iliyokubaliwa.

Idadi ya waliouawa wakati msongamano ulipotokea inaripotiwa kuongezeka na imefikia 20 kwa sasa nayo malalamiko yanawaandama waandalizi wa tamasha hilo.

Loveparade Duisburg 2010 Massenpanik Trauer NO FLASH
Mishumaa na maua ya kuwakumbuka waliopoteza maisha yao kwenye msongamano huko DuisburgPicha: AP

Tamasha hilo limekuwa likifanyika katika mji mkuu wa Berlin hadi mwaka 2006 lilipoanza kuhamishiwa miji tofauti ya Ujerumani.Tamasha la mwaka uliopita lilipangwa kufanyika mjini Bochum ila likafutwa kwasababu za kiusalama.Kulingana na muandalizi wa shughuli hiyo,Rainer Schaller,ili kuonyesha heshima kwa waliopoteza maisha yao,tamasha hilo halitowahi kufanyika tena