1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya Uli Hoeneß yagonga Vichwa vya Habari Nchini

11 Machi 2014

Kesi ya kukwepa kulipa kodi ya mapato mwenyekiti wa timu ya Bayern Munich,Uli Hoeneß, kutoweka ndege ya shirika la ndege la Malaysia na kumbu kumbu za balaa la kinuklea la Fukushima

https://p.dw.com/p/1BNDu
Uli Hoeneß katika ukumbi wa mahakama mjini MunichPicha: Reuters

Kesi ya kukwepa kulipa kodi ya mapato mwenyekiti wa timu bingwa ya ligi kuu ya Ujerumani Bayern Munich,Uli Hoeneß,kisa cha kutoweka ndege ya shirika la ndege la Malaysia na suala kama teknolojia ya kimambo leo itumike kutuliza hofu za kuzuka balaa Tunaanzia moja kwa moja mjini Munich ambako kesi ya mkuu wa timu bingwa,tajiri ya dimba nchini Ujerumani na miongoni mwa timu mashuhuri na tajiri kabisa ulimwenguni inaendelea katika ukumbi wa korti moja katika mji mkuu huo wa jimbo la kusini la Bavaria.Mpanda ngazi hushuka linaandika gazeti la "Badische Zeitung"Uli Hoeneß huyu, tunaemuona ameketi katika kiti cha mshitakiwa karika korti ya mjini Munich kwa makosa ya kukwepa kulipa kodi za mapato,hana tena kitisho cha mwenyekiti mwenye nguvu kupita kiasi wa timu ya FC Bayern Munich.Baada ya kufichua kwa mshangao wa wengi kwamba fedha alizokwepa kuzilipia kodi ni nyingi zaidi kuliko vile ilivyofikiriwa,atageuka kuwa mhalifu mkubwa zaidi miongoni mwa wahalifu wanaokwepa kulipa kodi nchini Ujerumani.Mtu anaweza kusema habadiliki huyu,akidhamiria amedhamiria.Hata kama anatambua fika kwamba safari hii anaujongelea zaidi mlango wa jela.

Majuto au Mbinu

Gazeti la mjini Weiden "Der neue Tag" linajiuliza kwanini hasa ameamua kufichua hata yale ambayo mwendesha mashtaka hakuwa akiyajua?Gazeti linaendelea kuandika:"Inamsaidia nini Honeß kufichua kwamba fedha alizokwepa kuzilipia kodi ni mara chungu nzima zaidi ya zile Euro milioni 3.5 zilizotajwa hapo awali?Sababu mbili zinaingia akilini:pengine ameungama kwasababu kweli anajuta kwa aliyoyafanya au pengine kuungama huko ni mbinu tu baada ya kuona hana pa kupita,bora apasue akitaraji adhabu haitakuwa kali.Na mengi yanaonyesha sababu hii ya mwisho ndiyo iliyomfanya aungame."

Prozessauftakt Uli Hoeneß Steuerhinterziehung 10.03.2014
Mwenyekiti wa Bayern Unich akizungukwa na polisiPicha: Reuters

Mada nyengine iliyogonga vichwa vya habari hii leo inahusu kisa cha kutoweka tangu jumamosi iliyopita ndege ya shirika la ndege la Malaysia iliyokuwa njiani kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing.Nini hasa kimetokea hakijulikani,nani wako nyuma ya kisa hicho hawajulikani.Gazeti la "Mittelbayerische Zeitung" linaleta uwiayo kati ya kisa hicho na chengine ambacho pia ni cha kuhuzunisha na kuandika:"Jumanne hii ya leo imekamilika miaka 10 tangu shambulio la kigaidi lilipofanywa dhidi ya treni ya abiria mjini Madrid na kuangamiza maisha ya watu 191.Shambulio ambalo polisi na watumishi wa idara za upelelezi hawakuwa waangalifu na wala kushirikiana.Katika majanga kama haya ndipo tunapotambua umuhimu wa kuwa na mfumo wa pamoja wa ushirikiano katika masuala ya usalama.

Miaka mitatu ya Fukushima

Na hatimae wahariri wamezungumzia balaa la kinuklea lililosababishwa na zilzala iliyozusha Tsunami huko Fukushima Japan na kujiuliza kama teknolojia ya kimambo leo isingesaidia kutuliza hofu zilizoko.Kumbukumbu za Fukushima,linaandika gazeti la "Rhein-Neckar Zeitung" la mjini Heidelberg:"Ni kweli kabisa kwamba nishati ya atomiki inazusha wasi wasi mkubwa zaidi nchini Ujerumani kuliko mahala kokote kule kwengine.Lakini kibaya kipi ikiwa teknolojia ya kimambo leo itatumika kuzuwia balaa lisitokee?Meli ya anasa ya Titanic ingekuwa bado pengine inata nanga katika bandari tofauti za dunia pindi wahandisi wangefikiria hadi mwisho.Pekee suala ambalo halijapatiwa jibu la wapi zizikwe takataka za kinuklea linabainisha hakuna njia mbadala ya kuepukana na nishati ya nuklea.

Fukushima 3 Jahre
Wafanyakazi wa kituo cha nguvu za umeme-TEPKO wamekusanyika kukumbuka miaka mitatu tangu Tsunami ilipopiga huko FukushimaPicha: Reuters

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri:Yusuf Saumu