1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi za waathiriwa wa baada ya uchaguzi Kenya

Amina Mjahid
17 Aprili 2019

Waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2017 nchini Kenya, wanaazimia kuishitaki serikali na asasi zake wakiwemo polisi kutokana na dhulma walizofanyiwa wakati wa ghasia hizo.

https://p.dw.com/p/3Gxz2
Kenia Unruhen nach Wahlen 2007/2008
Picha: Getty Images

Mashirika ya kijamii nchini Kenya yanaazimia kuishtaki mahakamani, serikali na asasi zake wakiwemo maafisa wa polisi, kwa niaba ya waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2017 nchini Kenya, kutokana na dhulma yanazosema walifanyiwa katika kipindi cha uchaguzi hasaa baada ya kutangazwa matokeo ya urais yaliyompa ushindi rais Uhuru Kenyatta.

Kiongozi wa kituo cha kijamii cha Kondele kinachojishugulisha na maswala ya haki Bonface Ogutu Akach anasema wameshirikiana na mashirika kadhaa kuwapa fursa waathiriwa wa ghasia hizo kutoka Migori, Siaya, Homabay na Kisumu kudai haki na fidia kutoka kwa serikali kutokana na madhila mbali mbali yaliyowafika yakiwemo ubakaji, majeruhi ya risasi na hata kupoteza mali.

Afisa wa shirika la kiislamu la haki za binadamu, MUHURI, Francis Auma amesema lengo la kuwaleta pamoja waathiriwa hao ni kukusanya ushahidi wa kutosha kuweza kuishtaki serikali.