1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Makubaliano ya amani ya Sudan yahatarishwa

13 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GF

Chama tawala kaskazini mwa Sudan,kimewakosoa washirika wake wa zamani waliojitoa serikalini. Chama cha NCP kimesema,uamuzi wa chama cha waasi wa zamani-SPLM kuwatoa mawaziri wake kutoka serikali ya umoja,unahatarisha makubaliano ya amani ya mwaka 2005.

Uamuzi huo pia umezusha wasiwasi kuwa mazungumzo ya amani yaliyopangwa kufanywa kati ya Khartoum na waasi kutoka jimbo la magharibi la Darfur huenda yakawa na utata.Mazungumzo hayo yanatazamiwa kufanywa baadae mwezi huu nchini Libya.Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika jimbo la Darfur,Jan Eliasson ameonya kuwa kuna hatari kubwa ya kuzuka machafuko mapya,ikiwa mazungumzo hayo yatacheleweshwa.