1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Muakilishi maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa matifa nchjini Sudan afukuzwa

23 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD00

Serikali ya Sudan imemfukuza mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Jan Pronk kutoka nchi hiyo. Jan Pronk alipewa siku 3 awe ameondoka.

Hatua hiyo ya viongozi wa Sudan imefuatia matamshi yake ya hivi karibuni kwamba majeshi ya serikali ya Sudan yalishindwa na waasi katika mapigano mawili yaliotokea mnamo miezi miwili katika jimbo lenye machafuko la Darfur, magharibi mwa Sudan.

Jan Pronk anatarajia kurejea mjini New York-Marekani kwa mashauriano na Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan. Sudan imepinga kutumwa nchini mwake wanajeshi 20,000 wa Umoja wa mataifa wa kulinda amani kuchukua nafasi ya wanajeshi kutoka Afrika 7,000. Wataalamu wanasema watu 200,000 wameshauawa na wengine milioni 2,5 kuyahama maskani yao tangu kuzuka mzozo wa kivita kati ya waasi na wanamgambo tiifu kwa serikali mwaka wa 2003.