1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM.China na Sudan kuimarisha uhusiano wa kibiashara

2 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVk

Rais Hu Jintao wa China ambae yuko ziarani barani Afrika ameafikia makubaliano ya kibiashara baina ya nchi yake na Sudan ambako aliwasili leo.

Nchi hizo mbili zimekubaliana kuimarisha uhusiano wake wa kibiashara licha ya jamii ya kimataifa kuishinikiza China itumie usuhuba wake na Sudan kuishawishi nchi hiyo ikubali hatua ya umoja wa mataifa ya kutaka kuingilia kati katika jimbo la Darfur huko magharibi mwa Sudan.

Wasaidizi wa rais Omar El Bashir wa Sudan wamesema kwamba China imetangaza kuwa itatoa mikopo ya mamilioni ya dola kwa Sudan.

China ikiwa na uchumi unaokua inafaidika kwa asilimia 60 ya kiwango cha mafuta yanayozalishwa Sudan.

Rais Hu Jintao anafanya ziara katika nchi nane za Afrika.