1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Mji wa haskanita watiwa moto

8 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Hg

Umoja wa mataifa umearifu kwamba mji wa Haskanita iliko kambi ya kikosi cha kulinda amani cha umoja wa Afrika ambayo iliyovamiwa na waasi wiki iliyopita umevamiwa tena na kuchomwa moto.

Wasimamizi wa umoja wa mataifa wameripoti pia juu ya kuporwa mali katika eneo hilo.

Taarifa ya pamoja ya umoja wa mataifa na umoja wa Afrika imesema kuwa raia wanaoishi katika eno hilo wamelazimika kuuhama mji huo.

Hakuna taarifa zozote zinazo eleza kuhusu waliohusika na uvamizi huo na serikali ya mjini Khartoum bado haijatoa tamko lolote.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka umoja wa mataifa ni kwamba mji wa Haskanita ulio chini ya usimamizi wa serikali umeteketezwa vibaya isipokuwa nyumba chache tu zilizosalia.

Kiongozi wa kundi la waasi la SLA Suleiman Jamous amesema watu kadhaa wameuwawa na wakati huo huo ameilaumu serikali ya mjini Khartoum kwa kuhusika na tukio hilo.