1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Suleiman Jamous huenda akasamehewa na serikali ya Sudan

9 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBai

Serikali ya Sudan imesema hii leo kwamba itaondoa kitisho cha kumkamata Suleiman Jamous ambaye ni muasi wakati mazungumzo ya amani yatakapomaliza mzozo katika jimbo la Darfur.

Jamous anatajwa kuwa mtu muhimu katika kuleta maridhiano kwenye eneo la mzozo la Darfur.

Jamous amekuwa akifungiwa kwenye hospitali ya Umoja wa Mataifa karibu na Darfur kwa zaidi ya miezi 13 baada ya Umoja wa mataifa kumsafirisha katika Hospitali hiyo kwa matibabu.Serikali ya Sudan haikufahamishwa juu ya hatua hiyo ya Umoja wa mataifa na kumtaja Jamous kuwa muhalifu.Serikali ya Sudan ilikuwa imesema itamkamata Jamous punde tu atatoka kwenye hospitali hiyo ya Umoja wa mataifa.Jamous ni mtu aliye na uungwaji mkono mkubwa wa makamanda wa waasi na kundi muhimu la waasi la SLA limetaka aondolewe kitisho cha kukamatwa kabla ya kuhudhuria mazungumzo ya amani na serikali yatakayoanza katika kipindi cha miezi miwili au mitatu.