1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kibarua kigumu kuhusu mzozo wa darfur

Jane Nyingi9 Julai 2007

Juhudi za pamoja kati ya umoja wa mataifa na umoja wa afrika kusimamisha mapigano katika eneo la darfur nchini Sudan zinayumbayumba kufuatia kuendelezwa kwa mashambulizi na waasi. Hali hii imewafanya wawakilishi maalum wa mashirika hayo kutilia shaka kuanzishwa kwa mashauri ya amani kati ya pande zinazozana mwezi ujao ambao ni muda wa mwisho uliotengwa.

https://p.dw.com/p/CHBH
wanawake na watoto katika kambi moja katika eneo la darfur wakisubiri msaada
wanawake na watoto katika kambi moja katika eneo la darfur wakisubiri msaadaPicha: AP

Miezi saba baada ya kuanza kibarua chao kuhusu mzozo wa darfur mwakilishi wa umoja wa mataifa Jan Eliasson na mwenzake wa umoja wa afrika Dr Salim Ahmed Salim wamepiga hatua chache tu katika kuyaleta pamoja makundi yanayozozana wakilalamikia kujikokota kwa makundi ya kutoa misaada na wachunguzi...

Hali hata imekuwa ngumu zaidi baada ya makundi matatu makuu ya waasi katika eneo la darfur kugawanyika na kuwa zaidi ya 12. Ni mapigano ambayo yamechochea hata uvujwaji wa sheria huko darfur.Dr salim Ahmed salim amabye ni mjumbe maalum wa umoja wa afrika kuhusu mzozo wa darfur anakiri kuwa si kazi rahisi

Wajumbe maalum katika mzozo huo wametenga mwezi ujao kama wa mwisho kuanzisha mashauri kati ya pande zinazozana. Na ili kufanikisha hayo yote wameitisha mkutano wa kimataifa tarehe 15 na 16 mwezi huu nchini libya ili kuzungumzia hatua walizopiga kufikia sasa.

Hata hiyo wachanganuzi wanasema wajumbe hao wangali na kibarua kigumu cha kujaribu kuyaleta pamoja makundi hayo mbalimbali ya waasi. Inakadiriwa zaidi ya watu elfu 200 wameuawa tangu mapigano hayo yalipoanza mwaka wa 2003 baada ya waasi kuchukua silaha kupambana na majeshi ya serikali kwa madai ya kubaguliwa kwa eneo lao.

Hali hii iliifanya serikali kuwapa silaha waasi wa Janjaweed kukabiliana na waasi hao. Marekani mara kwa mara imeyataja mauji hayo kuwa ya halaiki jambo linalokanushwa na serikali ya

khatoum kwa kusema ni watu elfu 9 pekee wameuawa.

Mashauri ya hapo awali yalichukua zaidi ya miaka miwili mjini abuja Nigeria na hakuna lolote liloafikiwa kati ya makundi hayo ya waasi. Na mgawanyiko huo umeendelea hadi sasa. Mashirika ya kutoa msaada yanasema mashauri yatakuwa magumu hadi usalama uimarishwe. Kumekuwepo na mashambulizi 30 hatua inayowatia kiwewe karibu wafanyikazi elfu 14 wa mashirika hayo cha kushambuliwa wakati wowote.

Taarifa nyingine ni kuwa kiongozi wa kikosi chenye mchanganyiko wa jeshi la kulinda amani la umoja wa afrika na umoja wa mataifa amesema Rodolphe Adada ana imani kuwa watafaulu katika kazi yao licha ya matatizo yaliyopo.

Adada ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya nje katika jamuhuri ya kidemocrasia ya congo alipewa jukumu la mwakilishi maalum wa umoja wa mataifa na umoja wa afrika katika mzozo wa darfur mwezi mei. Baada ya mazumgumzo rais Omar al bashir alikubali tarehe 17 mwezi juni kupelekwa kwa kikosi hicho kuchukua mahala pa kikosi kisichokuwa na vifaa vya kutosha cha umoja wa afrika.