1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV: Chama cha rangi ya chungwa chaongoza

1 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBL2

Nchini Ukraine chama cha upinzani cha rangi ya Chungwa kinacho elemea upande wa magharibi kinacho ongozwa na bibi Yulia Timoschenko kinaelekea kunyakua ushindi katika uchaguzi wa bunge ulioitishwa mapema wa mwishoni mwa wiki.

Huku asilimia sitini ya kura zikiwa zimehesabiwa mpaka sasa chama hicho cha rangi ya chungwa kinaongoza kwa asilimia 34 ya kura.

Chama cha majimbo yanayoelemea upande wa Urusi kinacho ongozwa na waziri mkuu anaeondoka Viktor Yanukovych kinafuata kwa asilimia 31 ya kura zilizo hesabiwa hadi sasa.

Chama cha Ukraine Yetu cha rais Viktor Yuschenko kimejipatia asilimia 16 ya kura.

Bibi Yulia Timoschenko anaetarajiwa kushinda katika uchaguzi huo amesema atakutana na rais Yuschenko kujadili juu kuunda serikali ya muungano.

Uchaguzi wa Ukraine uliitishwa mapema kufuatia mvutano wa ndani kati ya rais Viktor Yuschenko na waziri mkuu Viktor Yanukovych.