1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV : Mgogoro wa kisiasa wapamba moto

25 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByd

Mgororo wa kisiasa nchini Ukraine umezidi kupambana moto kufuatia kutimuliwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali nchini humo na Rais Viktor Yushchenko.

Svyatoslav Piskun ambaye ni mfuasi wa hasimu wa Yushchenko Waziri Mkuu Viktor Yanukovich ametimuliwa ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya kurudishwa tena kwenye wadhifa huo na ameapa kupinga amri hiyo.Wakati huo huo Rais amewaita mawaziri waandamizi na maafisa wa ulinzi kwa ajili ya mashauriano ya dharura.Waziri Mkuu Yanukovich naye ameetisha mkutano wa dharura wa baraza lake la wamaziri baada ya kuondoka kwa ghafla katika mkutano wa mawaziri wakuu wa majimbo ya Urusi ya zamani kusini mwa Ukraine.

Yushchencko amekuwa katika mapambano ya kuwania madaraka na Yanukovich tokea mwaka 2004 wakati mapinduzi ya chungwa yalipomuweka kwenye madaraka hayo ya urais.