1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV: Mzozo unatokota ndani ya siasa za Ukraine

3 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCw

Mzozo wa kisiasa unatokota nchini Ukraine.

Bunge la nchi hiyo limeapa kuendeleza vikao vyake licha ya rais Viktor Yuschenko kutoa agizo la kuvunjwa kwa bunge hilo na kufanyika uchaguzi wa mapema.

Azimio lililopitishwa katika mkutano wa dharura linapinga agizo la rais Yuschenko na kulifananisha na mapinduzi baridi, wabunge hao pia wamepinga matumizi kwa ajili ya kugharamia uchaguzi huo wa mwezi ujao.

Rais Viktor Yuschenko na waziri mkuu wake wametia saini agizo la kuvunjwa bunge la Ukraine na kutangaza tarehe 27 Mai kuwa ndio siku ya uchaguzi nchini Ukraine.

Rais Yuschenko mfuasi wa sera za magharibi amemlaumu waziri wake mkuu Viktor Yanukovych mfuasi wa sera za Kremlin kwa kutaka kuupanuza uwezo wake kwa kukiuka misingi ya katiba ya Ukraine.