1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV: Putin kuzuru Ukraine

22 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChL

Rais wa Urusi, Vladamir Putin, anatarajiwa hii leo kufanya ziara yake ya kwanza nchini Ukraine katika kipindi cha miaka miwili. Ziara yake inafanyika baada ya mzozo wa kibiashara na ugavi wa gesi kuzuka.

Rais Putin atafanya mazungumzo na rais wa Ukraine, Viktor Yuschenko aliyeongoza mapinduzi ya mwaka jana, na mawaziri wanaoongozwa na waziri mkuu wa Ukraine, Viktor Yanukovic, anayeiunga mkono Urusi. Ukraine ni njia muhimu kw agesi ya Urusi kwenda barani Ulaya.

Katika mazungumzo ya leo, Ukraine inatarajiwa kuishinikiza Urusi iondoe jeshi lake la wanamaji katika bahari nyeusi.