1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV: Wabunge wapitisha marekebisho ya sheria, Ukraine

2 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBve

Wabunge wa Ukraine wamekubaliana kufanya marekebisho kadha yanayohitajika kwa uchaguzi wa mapema.

Hatua hiyo imelengwa kumaliza mvutano wa madaraka uliopo kati ya Rais Viktor Yuschenko anayependelewa na mataifa ya magharibi na Waziri Mkuu Viktor Yanukovich anayependelewa na Russia.

Rais Viktor Yuschenko alikuwa ameongeza muda wa mwisho wa wabunge hao kuidhinisha sheria hizo kufikia saa sita za usiku wa kuamkia leo.

Wanasiasa hao wawili mwishoni mwa juma waliandaa kikao cha dharura na wakakubaliana kutenga tarehe ishirini na tano, Septemba kuwa siku ya uchaguzi wa mapema.

Wachunguzi wa maswala ya kisiasa walikuwa wamesema ghasia zingetokea nchini humo iwapo sheria hizo hazingerekebishwa.