1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV:Chama cha Upinzani chashinda kwenye uchaguzi wa bunge

1 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBL7

Chama cha upinzani kinachoelemea upande wa magharibi kimeridhika kuwa kimeibuka na ushindi wa uchaguzi wa bunge ulioitishwa mapema nchini Ukraine.

Kamisheni kuu ya uchaguzi imesema kambi ya mapinduzi ya rangi ya machungwa inayo ongozwa na bibi Yulia Timoschenko imejipatia asilimia 33 ya kura huku chama cha majimbo yanayo elemea upande wa Urusi kinacho ongozwa na waziri mkuu anaeondoka Viktor Yanukovitsch kikijipatia asilimia 31 ya kura.

Chama cha Ukraine Yetu cha rais Viktor Yuschenko kimejipatia asilimia 16 ya kura. Mshindi wa uchaguzi huo bibi Yulia Timoschenko aliyewahi kuwa waziri mkuu kufuatia vuguvugu la mapinduzi ya rangi ya machungwa mwaka 2004 ameeleza azma ya kuunda serikali ya muungano pamoja na chama cha Ukraine Yetu cha rais Viktor Yuschenko.

Waziri mkuu anaeondoka kwenye wadhfa wake Viktor Yanukovitsch ameelezea haja ya kuunda serikali ya muungano kwa ushirikiano pamoja na chama cha Ukraine Yetu na chama cha Kikomunisti.