1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kifo cha Seneta Edward Kennedy chaombolezwa duniani.

26 Agosti 2009

Viongozi wa dunia wamkumbuka Ted Kennedy.

https://p.dw.com/p/JIbj
Obama na KennedyPicha: AP

Risala za maombolezi kwa kifo cha Seneta Ted Kennedy wa Marekani, zinamiminika kutoka kila pembe ya dunia.viongozi mbalimbali kuanzia rais Barack Obama,rais wa zamani George Bush, mawaziri wakuu wa sasa na wa zamani wa Uingereza Gordon Brown na Tony Blair hadi waziri mkuu wa Australia, Kevin Rudd wametoa rambi rambi zao. Seneta Ted Kennedy,ndugu wa marehemu J.F Kennedy, amefariki dunia kutokana na maradhi ya kensa ya ubongo.

Rambirambi zimetoka kutoka takriban ulimwengu mzima juu ya Seneta huyu kutoka Massachusetts aliyefariki akiwa na umri wa miaka 77.Rais Barack Obama wa Marekani ambaye kuania kwake kuteuliwa mtetezi wa chama cha Democratc party mwaka jana kutiwa jeki mno kwa kuidhinishwa na Seneta Kennedy aliitoa rambi rambi zake mapema asubuhi ya leo kwa kusema : "Simba wa kutetea uhuru " ameaga dunia. Obama akasema na nnanukulu, "Ukurasa muhimu sana katika historia yetu umefungwa." Rais Obama alimwita Ted Kennedy, "Seneta mkubwa kabisa wa Marekani wa enzi yetu."Ufasaha wa Obama katika kuzungumza na heba yake mara nyingi ukifananishwa na ndugu mkubwa wa Ted Kennedy, Rais J.F.Kennedy,aliyeuwawa 1963.

Akitoa pongezi zake kwa ukoo wa marehemu : Rais Obama mara moja alisema:

"Kwa muda wa kiasi cha nusu karne,mke wa Seneta Edward M.Kennedy,ametoa mchango mkubwa kutupita sisi sote."

Nae Rais wa zamani wa Marekani, George Bush, kutoka chama cha wahafidhina cha Republican,alitoa nae rambi rambi zake kwa seneta Kennedy:Bush alisema na nnamnukulu:

"Wakati hatukuafikiana katika maswali mengi ya kisiasa miaka mingi iliopita,daima nikiheshimu utumishi wake usiotetereka kwa umma."

Bush alikumbusha kuwa alipongeza mchango wa Seneta Kennedy katika utumishi wa umma mwaka 2003 alpomtunza zawadii ya utumish bora wa wananchi: "Bush Award for Exellence in public Service". Marehemu Ted Kennedy akuhujumu vikali utawala wa Bush kama alivyosema wakati mmoja:Utawala huu umeleta uhasama zaidi na washirika wetu wa muda mrefu na badala ya kuifanya Marekani kuwa na usalama zadi,umeipunguzia usalama."

Seneta Tedd Kenndy altumika Baraza la senate akiwakilisha Massachusetts kwa miaka 47.

Kutoka nje ya Amerika, waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown, alisema ," Seneta Kennedy kifo chake kitaombolezwa sio tu nchini Marekani, bali katika kila bara."Brown akaongeza, Seneta Kennedy, anahusudiwa ulimwengu mzima kwa cheo chake cha "seneta wa maseneta".Aliongoza dunia katika kuhimiza usoni kabisa elimu kwa watoto na afya bora.Akaamini pia kila mtoto apewe nafasi ya kutimiza ndoto yake kikamlifu.

Mtangulizii wa Bw.Brown, Tony Blair alipongeza mchango mkubwa aliotoa marehemu katika kusimamia yale mazungumzo ya "Goood Frday" yaliiongoza amani katika Ireland ya kaskazini.

Waziri mkuu Benjamn Netanyahu wa Israel, akiwa njiani asubuhi ya leo kuzungumza na mjumbe wa Marekanii kwa Mashariki ya Kati George Mitchel,alimuita seneta Kennedy "Rafiki mkubwa wa dola la Israel".

Naye waziri mkuu wa Australia,Kevin Rudd alimwita Kennedy "Muamerika mashuhuri kabisa,mdemokrasia mkubwa na pia rafiki mkubwa wa Australia."

Mwandishi:Ali,Ramadhan /AFP/DPA/

Mahariri:Abdul-Rahman