1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kikao cha baraza la haki za binaadam la umoja wa mataifa

Oumilkher Hamidou3 Februari 2009

Ujerumani yakosolewa na wawakilishi 52 waloiohudhuria kikao hicho mjini Geneva

https://p.dw.com/p/GmCZ
Ujerumani yadadisiwa mjini GenavaPicha: picture-alliance / dpa / AP / Montage DW


Kwa mara ya kwanza kabisa baraza la Umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya haki za binaadam limejishughulisha na hali ya haki za binaadam nchini Ujerumani.Ujumbe wa watu 21 kutoka Ujerumani ulishiriki katika kikao cha baraza hilo mjini Geneva Uswisi na kutoa ripoti ya serikali kuhusu hali ya haki za binaadam humu nchini.Ujumbe huo ulihanikizwa kwa masuala na lawama za kila aina.


Ujerumani ni taifa linaloheshimu sheria na kuthamini sana haki za binaadam,wamesisitiza wawakilishi wa serikali kuu  mbele ya baraza la Umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya haki za binaadam,jana mjini Geneva.


Kwa namna hiyo  ujumbe wa serikali kuu ya Ujerumani ukiwa katika hali ya kujiamini kupita kiasi,umeweza kukabiliana na masuala yanayostahiki na hata lawama dhidi ya visa vinavyokiuka haki za binaadam vinavyosemekama vimetokea nchini Ujerumani.Bila ya upendeleo wala mabishano,wawakilishi kutoka mataifa yasiyopungua 52 walioshiriki katika kikao hicho cha Geneva walifafanua kwa kina visa vilivyotokea.Lawama zimetolewa kwa mfano dhidi ya kubaguliwa waumini wa kutoka jamii za wachache,visa vya matumizi ya nguvu vinavyofanywa na magengi ya siasa kali za mrengo wa kulia yenye hisia za chuki dhidi ya wageni ,ukosefu wa usawa kati ya watu wa jinsia ya kiume na wale wa jinsia ya kike na kukataa serikali kuu ya Ujerumani kutia saini makubaliano ya Umoja wa mataifa kuhusu haki za wafanyakazi wahamiaji.


Badala yake hali ya kuridhika ndio inayojitokeza linapohusika suala la haki za binaadam nchini Ujerumani,kama alivyolalamika mjini Geneva mkurugenzi wa taasisi ya haki za binaadam ya Ujerumani Heiner Bielefeld.Na hajakosea.Hata katika yale mataifa ambako haki za binaadam zinavunjwa kupita kiasi,sauti zimepazwa kuikosoa Ujerumani.


Kadhia kubwa zaidi ya kuvunjwa haki za binaadam ambayo Ujerumani inakosolewa kuchangia ni ile ya kujikinga  ulaya na wimbi la wakimbizi tangu  kati kati ya miaka ya 90,jambo ambalo linakwenda kinyume na makubaliano ya Umoja wa mataifa kuhusu wakimbizi.Katika wakati ambapo miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya Ujerumani inajitokeza kua nchi inayowapokea wakiimbizi wachache kuliko kwengineko,katika mipaka ya Umoja wa Ulaya na hasa katika eneo la bahari ya kati,maelefu ya watu wamekua wakipoteza maisha yao mnamo miaka ya hivi karibuni.Hakuna lakini nchi yoyote iliyezungumzia kadhia hiyo mjini Geneva,isipokua shirika la Amnesty International na mashirika mengine yasiyomilikiwa na serikali.