1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kikosi cha mipaka cha UU

21 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8V

BRUSSELS:

Katika juhudi za kuzima wimbi la uhamiaji Ulaya kinyume na sheria, mawaziri wa ndani wa Umoja wa Ulaya wameungamkono kuundwa kikosi cha kutumika haraka inapozuka dharura ili kuzisaidia nchi kama Spain kukabiliana na mminiko wa wahamiaji wasio halali.

Kikosi cha askari 450 wa mipaka kitatayarishwa panapozuka dharura ili kutumikia shirika la mipaka la UU Frontex.

Maafisa wa UU wamearifu kuwa ,kikosi hicho chaweza kuwa tayari ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Muitiko huu wa UU unaotokana na kuwasili kwa wahamiaji 31,000 katika visiwa vya Canary nchini Spain.Wengie 6.0000 walifariki baharini pale marekebu zao zilizosheheni zilipozama.