1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kikosi cha UNAMID huko Dafur

30 Julai 2009

Mwito watolewa na NGOs kusaidia UNAMID

https://p.dw.com/p/J0Px

Mashirika 22 yasio ya kiserikali (NGOs) miongoni mwayo "SAVE DAFUR COALITON", yametoa mwito ulimwenguni kutaka ziungwemkono juhudii za vikosi vya kuhifadhi amani vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afriika -maarufu (UNAMID) huko Dafur, mkoa wa magharibi wa Sudan.Kikosi hiki kimeshindwa katika hali nyingi za kutatanisha kwsa kuwa hakikupata msaada wa kutosha kutoka jamii ya kimataifa na kuendelea kukwamishwa na serikali kuu ya Sudan-mashirika hayo yamenungunika.

Hii ilikuwamo ndani ya taarifa yao ya pamoja iliotoa mapendekezo jinsi ya kuboresha kazi za kikosi hicho kilichoundwa miaka 2 iliopita.

Kikosi hicho cha mchangamnyiko kati ya UM na UA wakati huu hakina zana za kutosha kutekeleza jukumu lake la kuwalinda raia na hivyo kinashindwa kutekeleza wajibu wake mkuu .

Kwa mfano, helikopta zinazohitajiwa kwa uchukuzi bado hazikutolewa kwa kikosi hicho na serikali ya Sudan mjini Khartoum, inaendelea kukibana katika shughuli zake.

Pia hapo jana, Katibu mkuu wa UM Ban Ki-moon alisdema kuwa UNAMID huenda ikafikia idadii ya askari wake ya 26,000 mwishoni mwa mwaka huu,lakini kingali kina ukosefu wa zana muhimu mfano wa helikopta na vyombo vya usafiri wa shehena nzito.

Katibu mkuu akauwambia mkutano na waandishi habari katika makao makuu ya UM kuwa ni helikopta 6 kati ya zote 24 zinazohitajika zimepatikana na akazitaka kwa mara nyengine tena nchi zenye uwezo wa kutoa kuonesha nia ya dhati ya kisiasa .

Jukumu la mwaka mmoja la kikosi cha UNAMID linamalizika kesho ijumaa lakini linatarajiwa kurefushwa na baraza la Usalama la UM wiki hii kwa muda wa mwaka mzima mwengine.

Katika mapendekezo ya kujenga kikosi bora cha UNAMID, mashirika yasio ya kiserikali yamesema Marekani,Uingereza,Ufaransa na kanada zihakikishe juhudi mafunzo na zana zinawekwa usoni kuliko tafsri ya jukumu lililotolewa na kuwa uongozi huko Dafur unaongoza vikosi vya kijeshi na polisi ili kutimiza kikamilifu jukumu la kikosi cha UNAMID.

Mashirika hayo halkadhalika, yakaitaka serikali ya Sudan iwache haraka pingamizi zake katika shughuli za kikosi cha UNAMID .Pia nchii zenye ushawishi kwa serikalii ya Khartoum zihakikishe kuwa vikosi vya serikali ya Sudan na polisi wake pamoja na wanamgambo wao wanakoma kukiandama kikosi cha UNAMID na kukiruhusu kufanya kazi bila pingamizi kote mkoanii dafur.

jumuiya ya kimataifa nayo imetakiwa iheshimu jukumu lake katika kulipatia zana na uwezo wa kufanya kazi kikosi cha UNAMID.

Umoja wa Mataifa unakisia kwamba kiasi cha watu laki 3 wamefariki mkoani Dafur tangu waasi wa Dafur kushika silaha dhidi ya serikali kuu ya kaskazini inayodhibitiwa na wasudani wa asili ya kiarabu hapo 2003 wakilalamika kubaguliwa.Sudan inadai ni watu 10.000 tu waliopoteza maisha.

Mwandishi:Ramadhan Ali /AFPE

Mhariri:Mwadzaya Thelma