1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kila mtu ni mlengwa vita vya Sudan Kusini

Sekione Kitojo
24 Aprili 2018

Ripoti mpya inasema kila mtu na kila kitu ni lengo la mashambulizi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini, wakati  mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na  wafanyakazi  wa  kutoa  misaada yakiongezeka. 

https://p.dw.com/p/2wYzU
Südsudan Soldaten der Opposition
Picha: picture-alliance/AP Photo/S.Mednick

Ripoti  mpya  inasema  kila  mtu  na  kila  kitu  ni  lengo  la mashambulizi  katika  vita  vya  wenyewe  kwa  wenyewe nchini  Sudan Kusini, wakati  mashambulizi  dhidi  ya  vituo vya  afya  na  wafanyakazi  wa  kutoa  misaada yakiongezeka. 

Karibu  vituo  50  vya  afya  vilishambuliwa  mwaka  2016 na  2017, inasema  ripoti  hiyo  iliyotolewa  jana  na  kundi lenye  makao  yake  mjini  New York linaloangalia  hali  ya watoto  katika  mizozo  ya mapambano  ya  silaha. Katika karibu  matukio 750  katika  kipindi  kama  hicho  misaada ya  kiutu ilizuliwa  na  makundi  kadhaa  yenye  silaha, ikiwa ni  pamoja  na  majeshi  ya  serikali.

Majeshi  ya  wapinzani  pamoja  na  yale  ya  serikali yameharibu  kwa kudhamiria, kuchoma nyumba, kupora  na kukalia  majengo  ya  hospitali  na  vituo  vya  afya  na kuwakamata, kuwateka na  kuwauwa  wafanyakazi  wa hospitali pamoja  na  wafanyakazi  wa  mashirika  ya  kutoa misaada  kama  mbinu  ya  vita, kwa  mujibu  wa  ripoti hiyo, iliyoandikwa  kwa  misingi ya  mahojiano  ya  zaidi  ya watu  90 na  ambayo  ililenga  zaidi  upande  wa  majimbo ya  Greater Upper Nile, Bahr el Ghazal na  Equatoria.