1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Bunge ladai uchunguzi wa mapigano ya Kinshasa

7 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCC0

Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo hapo jana limedai ufanyike uchunguzi juu ya umwagaji damu wa mwezi uliopita ambapo kwayo mamia ya watu waliuwawa na pia limetaka wahusika wawajibishwe.

Katika kikao chake cha kwanza tokea wapiganaji wa kiongozi wa waasi wa zamani Jean Piere Bemba na vikosi vya Rais Joseph Kabila kupambana kwenye kitongoji vya Kinshasa spika wa bunge la taifa Vital Kamerhe ametaka uchunguzi ufanyike na wahusika wa ghasia hizo watambuliwe na kuadhibiwa.

Wapiganaji wa Bemba wametimuliwa mjini Kinshasa na tokea wakati huo Bemba amejichimbia kwenye ubalozi wa Afrika Kusiini akisubiri kusafirishwa kwa salama kupelekewa Ureno kwa matibabu.

Wanadiplomasia wa Ulaya wanakadiria kwamba idadi ya vifo kutokana na mapigano hayo ya tarehe 22 na 23 Machi ni kati ya watu 200 hadi 600.