1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Kiongozi wa upinzani alalamikia kunyimwa uhuru wa kuzungumza.

1 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD7F

Muungano mpya wa kundi la taifa katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo la mgombea mtarajiwa katika kuwania kiti cha urais Jean - Pierre Bemba siku ya Ijumaa umekishutumu chombo kinachoangalia vyombo vya habari nchini humo kwa kuwanyima uhuru wa kujieleza wawakilishi wa kundi hilo.

Mamlaka ya taifa ya vyombo vya habari imewazuwia wajumbe kadha wa muungano huo kutozungumza na vyombo vya habari, ambapo uundwaji wa muungano huo ulitangazwa rasmi siku ya Jumamosi, kwa matamshi ambayo yanasemekana kuwa yanachochea chuki .

Mamlaka hiyo pia imewazuwia baadhi ya waungaji mkono wa rais Joseph Kabila , ambaye anapambana na Bemba katika uchaguzi wa duru ya pili hapo Oktoba 29.