1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Mapigano yazuka tena.

8 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7He

Maafisa wa kundi la hifadhi ya wanyama la wildlife Direct wamesema kuwa waasi wamekamata eneo mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ambalo ni hifadhi ya taifa kwa ajili ya sokwe walioko katika hatari ya kutoweka. Mapigano makubwa ya makombora yalisikika kutoka katika makao makuu ya ofisi za msitu huo wa Virunga na walinzi wa mbuga hiyo walilazimika kukimbia.

Waasi ambao wanamuunga mkono jenerali muasi Laurent Nkunda wamekuwa wakipigana mara kwa mara na jeshi la nchi hiyo katika mbuga hiyo.