1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Mradi wa waziri mkuu Gizenga umeungwa mkono bungeni

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOj

Waziri mkuu mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,Antoine Gizenga,ameungwa mkono kwa wingi mkubwa bungeni kuhusika na mradi wa serikali yake.Lengo la mpango huo unaoitwa “Msingi Mpya“ ni kufufua uchumi wa nchi iliyoteketezwa kwa vita.Gizenga amesema,serikali inayotazamia kuanza kufanya kazi juma lijalo,itafuata sera ya kuwa na soko wazi,ikiwa ni pamoja na ubinafsishaji,kwa azma ya kuleta maendeleo katika sekta tano zilizopewa kipaumbele na rais Joseph Kabila.Hizo ni sekta za ajira,elimu,miundo mbinu,afya,maji na nishati.