1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Waasi wa Rwanda wasakwa Kongo.

29 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBx9

Jeshi la serikali ya jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo na majeshi ya kulinda amani ya umoja wa mataifa nchini humo yameanza kuwatafuta jana wanaosadikiwa kuwa ni waasi wa Rwanda ambao waliwapiga watu marungu na kuwakata kwa mapanga wanakijiji 17 na kuwauwa katika eneo la mashariki la jimbo la Kivu ya kusini mwishoni mwa juma.

Watu wengine 23 wamejeruhiwa na wengine zaidi ya 12 wametekwa nyara katika shambulio hilo la waasi, lililofanyika usiku wa Jumamosi dhidi ya vijiji vitatu katika eneo la Kanyola, kilometa 50 magharibi ya mji mkuu wa jimbo hilo wa Bukavu.

Maafisa wa umoja wa mataifa nchini Kongo wamesema kuwa wengi wa wahanga waliuwawa wakiwa wamelala. Baadhi ya wale waliotekwa wanafikiriwa kuwa wameuwawa.